Kuna Mafanikio ili Uyafikie; Lazima Ujifunze Kuidharau Aibu.
By Mwalimu Oscar Samba
Mimina Kitasa yaani Pigo Juu ya Utawala, au Ufalme Usioutaka yaani Uliodhalimu...
Ufunuo wa Yohana 16:1 Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
10 Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu.
Waombaji Wana nafasi Kubwa Sana ya Kuleta Mabadiliko Ktk Mifumo ya Uongozi Kwenye Maeneo Mbalimbali.
Uwokovu ni Vazi. Je, Unautunza Wokovu wako?
Nikuite Moyo hivi Leo kutokuendelea kucheza na Dhambi. Tunza wokovu, linda vazi lako. Yesu yu karibu kuja. Anakuja kulinyakuwa kanisa lake..
Ufunuo wa Yohana 22:13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
(Tuepuke Kuwatetea Watu, Kwa Kuwa Kwetu Ni Wema, Nakuziba Masikio Pale Wanaoonewa Wakilia.) Tuepuke Pia Kulazimisha Wanaokuonea Kuonekana Wabaya Kwa kila Mtu. By Mwalimu Oscar Samba
Ujumbee huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya Cha: KILI ZILIZO MACHO KATIKA UFALME WA MBINGUNI
Mathayo 24:45
Na Mwalimu Oscar Samba
Hiyo ni picha muhimu unayopaswa kuwa nayo, wakati huu unapoelekea kukisoma kitabu hiki. Ni muhimu sana kufahamu ya kuwa maana moja wapo ya Yesu ya kututaka tusilale usingizi yaani tuwe macho; ama tukeshe ililenga eneo la akili zetu.
Tazama mfano ule wa Wana Wali watano wenye Busara na watano Wapumbavu. Ndipo utakapotambua ya kuwa upumbavu unaotajwa pale, ni unaotokana na hali ya kutokujua ni nini cha kufanya katika nyakati kama hizi.
Malengo ya Kitabu:
1. Kuyafumbua Macho ya Aliyefumbwa, Kuziamsha Akili za Asinziaye ili Aweze Kuwa na Utayari wa Kutumika Kiusahihi (kama impasavyo), Katika Kulielekea Kusudi Aliloitiwa Kinyakati.
2. Kumpatia Ufahamu, Utakaotumika Vyema na Akili Zake, ili Kujua Ni Nini Kimpasacho Kukifanya Katika Majira Husika.
1 Mambo ya Nyakati 12:32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
3. Kumjengea Fikra za Kumuwezesha Kuzitambua Hila za Adui Shetani; Katika Mpango wa Kumnyamazisha au Kutaka Kumpoozesha Kiroho na Kiutumishi, (au Kiutumishi/Kiroho.) 2 Wakorintho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikra zake.
4....
Lengo Kuu: Kukujengea Fikra za Kiuamsho, Ili Kuibua Hari na Kuamsha .... Kukuumbia Nia ya Kiuamsho Ndani Yako. (Penye Nia, Pana Utayari).
.....,....
1. Maonevu na Migogoro Katika Kanisa, Ama Baina ya Watumishi, au Washirika: Ni Ishara ya Kujisahau Kiroho. Watu waliopoteza kusudi, au kulisahau ama walioshindwa kujitambua ndio pekee huweza kuanza kuumana. Unapoona
Na Mwl Oscar Samba
Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Lengo la Somo:
Kukuwezesha, au Kukujengea Fikra za Kuhitaji Msaada Wa Roho Mtakatifu; Ili Awe Mwezeshaji Wako Mkuu, Katika Kulipa Gharama kwa Ajili ya Uamsho.
Taswira ya Ujumbe: Imejikita katika kufahamu umuhimu wa kumpata Roho Mtakatifu kipindi cha maandalizi ya kiroho kwa ajili ya uamsho. Hapa nilipo nalenga aina ya upako unao hitajika, ili kulipa gharama ya kuleta Uamsho. Ni sawa na kipindi kile cha mwanafunzi kusoma kabla ya kazi. Uamsho ni kipindi cha kazi, lakini kabla ya kazi kilipita kipindi aidha cha chuo au shule.
Askari kabla ya kuingia vitani, au kuwa askari kuna kipindi cha mafunzo au cha maandalizi ya vita. Sasa kipindi hiki katika swala la Uamsho, ndicho hukiita kipindi cha kulipa gharama kwa ajili ya Uamsho.
Kati ya eneo kubwa na muhimu watu wengi hawalijui wala kulizingatia, ni lile la maandalizi au la kulipa gharama. Mfano, Uamsho wa huduma ya Yesu, ulilipwa gharama na watu wengi. Akiwemo Yohana Mbatizaji, aliyekaa nyikani akila asali ya mwitu na nzige. Akivaa mavazi kama ya Elia, yaliyo ya ngozi na kadhalika. Maana huyu alikuwa ni mtangulizi.
By Mwalimu Oscar Samba
Shalom Mtu wa Mungu, Karibu katika Makala hii, ikiwa ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha JIFUNZE KUMUAMINI ROHO MTAKATIFU KATIKA HILO ENEO*..
Na Mwl Oscar Samba
Katika Badiliko la Tabia
. Unageuzwa/Hutugeuza Na Kutupa Maisha Mapya . Dhambi ilipoingia ulimwenguni ilitupatia mwili wenye tabia au vinasaba vya chembechembe za dhambi. Ile mauti iliyonenwa, iliua sehemu kubwa ya asili au ya tabia ama ya vinasaba vya Kiungu katika maisha yetu. Na badala yake, tukatwa asili ya Shetani. Ndiposa kuna kitu Paulo hukiita utu wa kale, pia tabia za mwilini ama mwili huu wa tamaa ama tamaa za mwili. Ndiposa suluhu hutajwa ni kuokoka, ili uwe au uusulubishe mwili wako pamoja na Kristo pale msalabani. Waruni 5-8, na Wagalatia 5 inatusaidia sana katika hili.
Paulo anatufundisha sana kuwa, Yesu alipokuwa anakufa, aliufia mwili wa dhambi. Yaani mauti yake, ilikuwa inauwa asili ya Shetani katika miili yetu; japo kwa lugha ya Kibiblia neno nguvu ya mauti, au utawala wa mauti katika miili yetu linaonekana kutumika zaidi. Kwa lugha nyingine tunasema mfumo wa dhambi. Lile andiko la tulio wa Kristo hatutendi dhambi (1 Yohana 3:6, 8, 9; "ukisoma utakuna na neno mbegu, tafakari kwa kina neno hilo" wa 10, 'unakupa matokeo:') maana yake, tuliookoka hatupo au hatutawaliwi na mfumo au utawala wa dhambi. Ikimaanisha nguvu ya mauti, au mauti twajua ni nguvu ya Shetani kupenyeza dhambi.
Soma; Waebrania 2:14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Mada ya Kwanza Katika Kitabu Chetu Kipya cha Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo...
Na Mwl. Oscar Samba
1.Ushuhuda
Chimbiko kuu la kitabu hiki ni tukio binafsi lililonikuta, ambalo moja kwa moja Roho Mtakatifu alilitumia kama somo ili kunivusha mahali lakini pia kwa nia ya kupangua baadhi ya mienendo isiyo sahihi katika njia zangu. Iwe ni za kihuduma au kimaisha kama vile uchumi, kijamii na kadhalika.
Somo hili nimelipata katika mradi ninaoufanya wa kutotolesha vifaranga vya kuku na ufugaji. Siku ya 21 ilipofika, vifaranga vikaanza kuanguliwa; kikanuni ni hadi kitoke kwenye kasha lake, kikauke ndipo ukitoe kwenye mashine.
Mimi vilipoanza tu kutoboa kasha, (eneo la kichwa) nililazimisha kumenya kasha zima. Hali iliyovipelekea kufa maana nilikuja kugundua ya kuwa eneo la kichwa ndilo hutangulia, na maeneo mengine hufuatia kwa kuendelea kukomaa au kukauka au kujiunda na humalizikia mkiani. Sasa ukikimenya pale mwanzoni, unakifanya kife maana maeneo hayo mengine yanakuwa bado hayajafikia muda wake wa kukamilika.
Baya zaidi, yale mayai ambayo yameshaanza kumenyeka au kupasuka eneo la kichwa, niliyachukua baadhi (yaliyoelekea sana) na kuyapeleka eneo la kukuzia vifaranga. Hapo nikaja na kukuta vyote vimekufa kwa kuzidiwa na joto! Lo! Nikajifunza kitu.
Kati ya funzo moja wapo la Kibaolojia ni kwamba, elimu ya kifizikia iliyotumika kutengeneza mashine ya kuatamieshia, imeundwa katika mfumo wa joto lililopangwa (mfano kwa vifaranga kwangu naweka 37.8) kuwa na uwezo wa kutoongezeka. Yaani halipandi kiasi cha kuadhiri mayai au vifaranga. Kwanza kuna feni na kuna hali ya unyevunyevu, pamoja na vifaa vilivyotumika kutokupata joto.
Utangulizi wa Kitabu Chetu Kipya Cha_ Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo ....
Na Mwl. Oscar Samba
Utangulizi
Tumekuwa na utamaduni mkubwa sana wa kutegemea akili zetu bila kufahamu umuhimu wa kumtegemea Roho Mtakatifu. Ni kweli akili na fahamu zetu ni kiungo muhimu katika kuyaendesha maisha yetu. Ila Kibiblia mwanadamu hakuumbwa kuzitegemea, badala yake aliumbwa kumtegemea Mungu, ingawaje aliumbwa kuzitumia akili; tena Paulo mtume anamtaka azitumie ipasavyo. Kwake sio kuzitumia tu, bali ni ipasavyo. Utafiti mmoja rasmi uliwahi kuonyesha kuwa, bara fulani ulimwenguni watu wake tunatumia asilimia tano tu ya ubongo wetu. Natumai hii ni sehemu au chachu kubwa ya hali duni ya maisha tuliyonayo.
Lakini tena na tena, yote katika yote; ni kwamba akili za mwanadamu ziliumbwa zifanye kazi kwa msaada wa Kiungu. Ni dhambi tu ilivuruga eneo hili, na kumfanya mwanadamu kuishi kana kwamba
Na Mwl Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA, Tunachambua kila Tukio Muhimu la Kiuamsho Katika Biblia.
Somo la .... SIFA NA KUABUDU KATIKA KWELI; Maneno Yenye Uhalisia Katika Kumuabudu au Kumsifu Mungu.
Licha ya umuhimu wa hali ya kiroho ya mtu anayemsifu au kumuabudu Mungu, ambapo tunaongozwa na lile andiko la Zaburi linalotutaka tuwe na moyo safi ( Zaburi 33:1 Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Rejoice in the LORD, O ye righteous: for praise is comely/inatoka for the upright.); lakini pia uteuzi wa maneno na muundo wa sentesi zetu katika kumuimbia Mungu: lazima visadifu uhalisia.
Lazima yataje aidha ukuu wa Mungu, uweza wake au utukufu na utakatifu wake. Tabia zake na utendaji wake uliotukuka vinapaswa kuwa ni sehemu ya maneno yaliyoteuliwa na mtunzi sanjari na muimbishaji wa wimbo.
Tuna nyimbo nyingi leo zinaitwa za kuabudu ni kwa sababu tu zinaimbaa katika hali ya utulivu. Na zile za kusifu ni kwa sababu zinaimbwa kanisani na katika hali ya kuchangamka. Hatusifu kwa kuwa wimbo unamsifu Mungu, bali ni kwa kuwa muimbishaji katuambia tusiamame tumsifu Mungu. Ni kwa kuwa mpigaji kapiga mapigo yakutuchangamsha.
Na Mwalimu Oscar Samba
Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA
Tunachambua kila Tukio Muhimu Katika Biblia Nzima, hususani lile lenye Ujumbe wa Kiuamsho Ndani Yake.
Kitabu cha Kutoka, Sura ya 13 na 14
Somo la .... KUVUKA BAHARI YA SHAMU: Ushindi Katika Mlango wa Msimu Mpya Kihuduma au Kimaisha.
Msimu Mpya maana yake ni mabadiliko au hatua nyingine mpya ya kimaisha, na hata kihuduma yaani kiroho. Mabadiliko haya huanzia rohoni kweli, ila huwa na matokeo katika maisha ya uhalisia ya mwilini. Kabla ya kuingia msimu huo mpya, unahitaji kupita katika lango la msimu. Hapa ndipo huwa na upinzani mkubwa sana. Mwanafunzi yeyote lazima awe makini na kipindi chake cha mitihani. Na kuna wengine kipindi hicho huwa katika mashambulizi sana. Ni kwa nini? Ni kwa sababu kuingia kwake katika hatua nyingine, kunategemea kuvuka kwake katika mtihani huo.
Wana wa Israel walikuwa wanaingia katika msimu wa maisha mapya. Kiuchumi tungeuita sekta isiyo rasmi. Maana ile ya jangwani tunaiita ni sekta ya umma. Walilishwa na serikali, na kuhudumiwa na wao. Jangwani wanajiandaa kuishi maisha ya ndege wa angani, yaani sekta isiyo rasmi. Hapo wanalishwa na MUNGU mwenyewe kwa njia ya muujiza.